JE UNAMJUA UNAYESHINDANA NAYE USIKU NA MCHANA?
KABLA ULIMWENGU KUUMBWA SHETANI ALISHATUPWA DUNIA
“Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi.” Mwanzo 1:1,
“Ulikuwa wapi nilipo nilipoiweka misingi ya nchi? Haya sema kama ulikuwa na ufahamu.Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake kama ukijua ?” Ayubu 38:4-7
Kabla ya Mungu kuumba ulimwengu huu malaika walikuwepo ikimaanisha Lucifer (maana yake Nyota ya asubuhi inayo ng’aa) alikuwepo kabla hatujakuwepo pamoja na malaika zake wote walikuwepo.
“Naye alituokoa katika ufalme wa giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani msaamaha wa dhambi…kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa,vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi..” Wakolosai 1: 13-16
Sasa turudi nyuma: Malaika ni nani?
Malaika ni roho iliyoumbwa na Mungu kwa ajili ya kumtumikia Mungu,kumbwabudu na kumtii Mungu kwa sababu kwa yeye vitu vyote viliumbwa.Malaika hawaonekani kwa macho kwa sababu hawana mwili kwa maan wao ni roho,japokuwa wameonekana kutajwa katika biblia kuonekana mbele za wanadamu.
Kumbuka biblia haisemi kuwa watu huwa malaika pindi wanapokufa,pia haizungumzii chochote kuhusu malaika watoto.
Japokuwa malaika ni viumbe waliumbwa hawakuzaliwa ndio maana hawana uwezo wa kuzaliana wala hawaitaji kuzaliana, na sababu hii inadhibitisha kuwa shetani na malaika zake hawana uwezo wa kuongezeka watabaki walivyo mpaka mwisho wa ulimwengu..Kumbuka shetani ni malaika Mkuu aliyekuwa na kundi la malaika wadogo wanaomtumikia. Pia biblia haizungumzii chochote kuhusu malaika wa kike..Wala hawana haja ya malaika wa kike kwa kuwa malaika hawafi wanaishi milele..kuwa makini sifa zote zitakazotajwa humu ndani kama sifa za malaika sifa hizo shetani na malaika zake wanazo pia vile vile..Pengine watu wengi wamekuwa wakitafsiri uwepo wa malaika wa kike kwa sababu mwanamke ni mtulivu Zaidi kuliko mwanamme,lakini sio kila biblia ina sema ila ni kile watu wanafikiri tu.
Kipindi masudukayo walipo mfuata Yesu na kumuuliza kuhusu habari ya mwanamke aliyekuwa na waume wengi,siku ya kiama atakuwa mke wa nani? Yesu aliwajibu hatakuwa mke wa yeyote kwa kuwa hakutakuwa na kuoa wala kuolewa kwa kuwa watakuwa kama malaika wa mbinguni..Mathayo 22:23-30
Turudi nyuma tena Mwanzo 1:1-2 “Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi.Nayo nchi ilikuwa ukiwa na utupu, na giza lilikuwa juu ya vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.”
Soma tena Jeremia 4:23-26 “Naliiangalia nchi,na tazama ilikuwa ukiwa,haina watu;naliziangalia mbingu, nazo zilikuwa hazina nuru…hapakuwa na mtu hata mmoja,na ndege wote wa angani wamekwenda zao..na miji yote ilikuwa imebomolewa mbele za Bwana” Hebu tazama hapa miji,ndege na mtu wanatajwa kutokuwepo na kusababisha ukiwa na utupu wa ulimwengu..kama hapakuwa na mtu ni nani alijenga hiyo miji?
Biblia haizungumzii haya yote kwenye kitabu cha mwanzo ila malaika walikuwepo wakishangilia na Mungu ulimwengu ulipoumbwa, japo uumbwaji wao haujaelezewa kikamilifu kwenye biblia.
Luciferni malaika aliyekuwa karibu na Mungu ila alimsaliti Mungu kwa sababu ya kutaka utukufu.Alitaka kuwa kama Mungu alitaka amupindue Mungu na kuchukua nafasi yake.
Baadae alipewa jina la Shetani likiwa na maana ya mpinzani
Isaya 14:12-17 “Jinsi ulivyo anguka kutoka mbinguni,Ewe nyota ya alfajiri,mwana wa asubuhi. Jinsi ulivyokatwa kabisa,ewe uliye waangusha mataifa. Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti change juu kuliko nyota za Mungu; nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano…lakini utashushwa mpaka kuzimu; mpaka pande za mwisho za shimo….aliyeufanya ulimwengu ukiwa,akaipindua miji yake;…”
Nafikiri sasa unapata picha ya kwa nini shetani alikuwepo kwenye bustani ya edeni hapo mwanzo.
Ezekieli 28:2,12-19 “…,kwa kuwa moyo wako umeinuka, nawe umesema Mimi ni Mungu,nami nimeketi katika kiti cha Mungu…,12…umejaa hekima,na ukamilifu wa uzuri.Ulikuwa ndani ya Adeni(Hii ni bustani ambaye mfano wako ni bustani ya Edeni iliyokuwa duniani,kwa kuwa Mungu alitaka tuishi maisha ya mbinguni tukiwa duniani hili ni somo jingine),bustani ya Mungu ,kila jiwe la dhamani lilikuwa kifuniko chako..; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako, katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari.Wewe ulikuwa kerubi (kerubi ni malaika wenye nguvu sana wao ndo wale malaika wenye sura nne, ya ndama,simba,tai na binadamu,hawa ndo wanaitwa wenye uhai wane..nafikiri unaelewa sasa shetani ni nani na ana nguvu kiasi gani) mwenye kutiwa mafuta(kutiwa mafuta-kuchaguliwa-kuwa juu ya wengine- kupendwa Zaidi.) afunikaye;nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu,umetembea huko na huko kati yam awe ya moto.Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako….nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme(wewe na mimi ni wafalme tutawalao pamoja na Kristo-kulazwa mbele yetu-ni nani akaaye chini mbele ya mfalme kama sio mtumwa wa mfalme..sasa shetani hakukaliswa chini mbele yetu alilazwa mbele yetu..)….umepatia unajisi patakatifu pako;(shetani anajua sharia na taratibu za Mungu kuliko wanadamu tujuavyo-watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa)”
Maswali ninayo kuacha nayo leo :
2. Je, akitokea kwako na sura tofauti na hiyo unayotegemea utamjuaje?
Tukutane muda mwingine katika muendelezo wa somo hili.
Na Mungu aliye Mbinguni, aliye juu sana ambaye pindo la vazi lake limefunika hekalu, akulinde mpaka tutakapokutana tena upate ufahamu Zaidi ili uwe na hekima juu ya maamuzi yako.
By. Your Servant. Emmanuel M. Mhombwe
No comments:
Post a Comment