IJUE BIBLIA | LISTENING GOD'S VOICE THROUGH GOSPEL SONGS


Breaking News

Saturday 7 September 2019

SALA YA BWANA

IJUE BIBLIA | KNOW THE BIBLE

SALA YA BWANA

-Je Unajua Maana Yake Na Unaisalije Sala Hiyo?-



BWANA YESU ASIFIWE!
UTANGULIZI:

Sala ya Bwana, ambayo pia huitwa Baba Yetu (Kilatini, Pater Noster), Ni Sala ya Kikristo ambayo, kulingana na Agano Jipya, Yesu alifundisha wanafunzi wake kama njia ya kuomba:

                                          Pray then in this way ... (Matthew 6:9 NRSV)
                                          When you pray, say ... (Luke 11:2 NRSV)

Matoleo mawili ya sala hii yamerekodiwa katika injili: sala ambayo ni ndefu ndani ya Mahubiri ya Mlima katika Injili ya Mathayo, na sala ambayo ni fupi katika Injili ya Luka wakati "mmoja wa wanafunzi wake akamwambia, 'Bwana, tufundishe kusali, kama vile Yohana alivyofundisha yake wanafunzi. '"(Luka 11: 1 NRSV).
Sala hii imegawanyika katika maombi saba,
Vifungu saba vya Sala hii ni kama ifuatavyo:
1               .      Baba yetu uliye mbinguni
2               .      Jina lako litukuzwe.
3               .      Ufalme wako uje,
4              .      Mapenzi yako yafanyike hapa duniani kama huko mbinguni.
5              .      Utupatie leo riziki yetu ya kila siku.
6               .      Na utusamehe makosa yetu kama sisi tulivyokwisha kuwa samehe waliotukosea.
7               .      Na usitutie majaribuni, bali utuokoe kutokana na yule mwovu,

Maombi matatu ya kwanza kati ya saba kwenye Mathayo yanamuongelea Mungu;
mengine manne yanahusiana na mahitaji ya binadamu,msamaha(upendo) na usalama wake.

Matthew 6:9-13 (RSV-2CE)
Luke 11:2-4 (RSV-2CE)
Basi msalipo ombeni hivi:
‘Baba yetu uliye mbinguni jina lako litukuzwe. 
10 Ufalme wako uje, mapenzi yako yafanyike hapa duniani kama huko mbinguni. 
11 Utupatie leo riziki yetu ya kila siku. 
12 Na utusamehe makosa yetu kama sisi tulivyokwisha kuwa samehe waliotukosea. 
13 Na usitutie majaribuni, bali utuokoe kutokana na yule mwovu,’
Akawaambia,
“Mnapoomba, semeni hivi: Baba, Jina lako litukuzwe; Ufalme wako uje. 
Utupatie chakula chetu kila siku. 
Utusamehe dhambi zetu kwa kuwa na sisi tunawasamehe wote wanaotukosea. Na usitutie katika majaribu.”

Baadhi ya mamlaka zinaongeza, kwa namna fulani, ‘Kwa kuwa ufalme ni wako na nguvu na utukufu, hata milele. Amina.’
MAFUNDISHO NA UCHAMBUZI:
Katika mafungu hayo saba kama tulivyoona hapo juu, vimegawanywa katika makundi makuu mawili:
1.      Linamzungumzia Mungu
Ø  Ubaba wa Mungu
·         Kwanini iwe Baba yetu na sio Mungu wetu?
"Yetu" inaonyesha kuwa sala ni ile ya kikundi cha watu ambao hujiona kuwa watoto wa Mungu na ambao humwita Mungu "Baba" yao.

Rum 8: 14-16,
14 Kwa maana wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu ni wana wa Mungu. 15 Hamkupewa Roho anayewafanya kuwa tena watumwa wa hofu. Lakini mmepokea Roho anayewafanya kuwa wana. Na kwa Roho huyo tunaweza kumwita Mungu, “Abba! Baba!” 16 Ni Roho mwenyewe anayeshuhudia pamoja na roho zetu kwamba sisi ni wana wa Mungu.

Rum 4: 1,17,
4 Tusemeje basi kuhusu baba yetu Abrahamu? Yeye alijifunza nini?
17 Kama ilivyoandikwa: “Nimekufanya wewe kuwa baba wa mataifa mengi.” Yeye ni baba yetu mbele za Mungu aliyemwamini. Mungu ambaye ana wapa wafu uhai na ambaye huamuru vitu ambavyo havipo viwepo.

Marko 14:36,
36 Akasema, “Aba, Baba, mambo yote yawezekana kwako. Tafadhali niondolee kikombe hiki cha mateso. Lakini si kama nitakavyo mimi, bali mapenzi yako yatimizwe.”

Galatia 4: 5-6,
ili kusudi awakomboe wale waliokuwa chini ya sheria, tupate kibali cha kuwa wana wa Mungu. Na kwa kuwa ninyi sasa ni wana wa Mungu, Mungu amemtuma Roho wa Mwanae akae ndani ya mioyo yenu, akiita, “Abba! Baba.”

Efeso 1:2,3
Nawa takieni neema ya Mungu na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Asifiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ametu bariki sisi kwa kila baraka za kiroho zitokazo mbinguni tukiwa ndani ya Kristo.

Efeso 2:2,3
Hapo zamani mliishi maisha ya jinsi hiyo, mkimtii mfalme wa nguvu za anga, ambaye ndiye ile roho inayowatawala wote wanaomwasi Mungu. Sisi sote pia tuliishi miongoni mwao hapo zamani, tukiridhisha na kutawaliwa na tamaa mbaya za mwili na mawazo. Kwa hiyo sisi pia tulikuwa kwa asili tunastahili ghadhabu ya Mungu kama binadamu wengine wote.

Elezea Baba yako anasifa gani tofauti na baba yako mzazi wa duniani.

Wewe mtu! Mwambie mfalme wa Tiro kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Wewe una kiburi cha moyo, na umesema kwamba wewe ni mungu, kwamba umekalia kiti cha enzi cha miungu, umekaa mbali huko baharini. Lakini, wewe ni binadamu tu wala si Mungu, ingawa wajiona kuwa una hekima kama Mungu- Ezekieli 28:2

Duniani kuna Miungu mingi sana toka enzi za mababu ambayo sisi binadamu tumeiabudu na kuitumikia kwa kujua ama kutokujua, Mungu hapendi afananishwe na miungu yako ndio maana anataka mahusiano zaidi na wewe ya ubaba na sio Mungu, maana Baba ana masharti yake si sawa na ya Uungu wake,kama Baba yako unaweza kuomba hata vitu vidogo vidogo ambavyo pengine wahisi labda si vya kumuomba, mfano:

Mathayo 7
“9 Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe? 10 Au akiomba samaki, atampa nyoka? 11 Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu zawadi njema, je! Si Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema zaidi wao wamwombao?”

Unaweza kuomba hela ya daftari kama wewe ni mwanafunzi, vitafunwa vya asubuhi, nazungumzia mahusiano uliyonayo wewe na baba yako kiasi cha kumueleza kwamba baba kalamu yangu imeisha. Haya ndio anayataka Baba yako aliye mbinguni, angalia hapo juu kwa makini ‘mkate’ na sio nyumba au gari au mali, ‘samaki’ na si kama wewe uwazavyo kwamba mpk uombe ada au shida kubwa kwelikweli.
Alilisha watu maelfu wa Israel jangwani, na wayahudi nyikani, wewe mmoja atashindwa, mwambie Baba, viatu vya shule vimeisha, sare imechakaa, sina begi, kwanini ulale njaa huna chakula, kwanini ulale chini kisa huna godolo na kitanda, mwambie baba yako aliyeko mbinguni acha kupata tabu wakati unababa ana uwezo.


LITAENDELEA WIKI IJAYO ...............................................

  •  Kwanini mpaka tuseme uliye mbinguni?Mpaka kufikia hapo tumezunguzia kipengele kimoja tu cha Baba yetu ,naomba ndugu mpendwa kama una swali, maoni ama unahitaji kushiriki katika maombi usisite kuwasiliana nasi kupitia 
  • ukurasa wa mawasiliano-contact us tuma barua pepe yako ikiwa na namba ya simu nasi tutakupigia simu
  • maoni tuandikie kwenye comment box hapo chini

No comments: