IJUE BIBLIA | LISTENING GOD'S VOICE THROUGH GOSPEL SONGS


Breaking News

Showing posts with label MWALIMU MWAKASEGE. Show all posts
Showing posts with label MWALIMU MWAKASEGE. Show all posts

Sunday, 7 October 2018

October 07, 2018

JIFUNZE KUSAMEHE NA KUSAHAU - MWALIMU CHRISTOPHER MWAKASEGE

JIFUNZE KUSAMEHE NA KUSAHAU - MWALIMU CHRISTOPHER MWAKASEGE



    JIFUNZE KUSAMEHE NA KUSAHAU
    Tuna uhakika ya kwamba, Roho Mtakatifu anakuongoza kusoma somo hili kwa makusudi kamili. 

    Maneno yaliyomo humu ni ya kukusaidia wewe na Wakristo wote, ili tuweze kuishi maisha ya "amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao."(Waebrania 12:14). 
    Kusamehe na kusahau ni tatizo kubwa ambalo limewazuia wakristo wengi wasipokee majibu ya maombi yao toka kwa Mungu. Ninaamini kuwa maneno yaliyomo humu yatakusaidia katika kupokea majibu ya maombi mengi ambayo hujayapokea. 


    Ni maombi yetu kwa Mungu, katika Jina la Yesu Kristo ya kwamba, Roho Mtakatifu ayachukue mafundisho haya na kuyaandika katika moyo wako, na akusaidie kuyatenda. 
    Na unaposoma itakuwa ni vizuri ukiwa na Biblia yako karibu, ili usome mistari yote tuliyoiandika. Somo hili tutajifunza kwa wiki sita mfululizo. Somo la wiki inayofuata litakuwa linajenga juu ya somo la wiki linalotangulia hasa baada ya wiki ya kwanza. 
    Mungu akusaidie unapofuatilia somo hili mpendwa wa mungu 

    KUTOKUSAMEHE NI KIKWAZO
    " Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. Lakini kama ninyi hamsamehi, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu" (Marko 11:25,26). 


    Kutokusamehe ni kikwazo na kizuizi kikubwa ambacho kinasimama kati ya mtu na majibu ya maombi yake. Watu wengi wanapenda imani zao zikue, lakini kwa sababu ya kutokusamehe imani zao zinakuwa hazina matunda. 
    Tatizo si kwamba watu hawapendi kusamehe. Ingawa watu wanapenda kusameheana, lililo wazi ni kuwa walio wengi hawajui namna ya kusamehe kule kunakokubalika na Bwana. Watu wengi wanajifunza katika biblia juu ya imani, maombi, utakatifu na mambo mengine ya kiroho. Lakini ni watu wachache wanaojifunza kutoka katika biblia namna ya kusamehe.Kati ya vizuizi vya mtu kupokea jibu la maombi yake kutoka kwa Mungu, ni tatizo la kutokujua jinsi ya kusamehe. 
    Bwana Yesu alipowambia wanafunzi wake juu ya kusamehe alitaka waone uhusiano ulipo kati ya sala na kusamehe. Kwa maneno mengine alitaka wafahamu kuwa kujibiwa kwa maombi na sala na dua kunategemea sana uhusiano walionao na watu wengine.Kabla Yesu hajasema juu ya kusamehe alizungumza maneno muhimu sana juu ya maombi. Yesu alisema hivi: 

    " Mwamini Mungu. Amini, nawaambia, yeyote atakayeuambia mlima huu, ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake. Kwa sababu hiyo nawaambia, Yoyote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu." (Marko11:22 - 24) 

    Haya ni maagizo muhimu sana kwa kila mkristo, kwa ajili ya maisha ya ushindi kila siku. Na watu wengi wamekuwa wakiitumia mistari hii, ili kupata mahitaji yao ya kiroho na ya kimwili. 
    Mafanikio yako katika kutumia mistari hiyo na ahadi hizo za Bwana Yesu, yatategemea sana jinsi wewe unavyofuata maagizo ya Yesu juu ya matumizi ya mistari hiyo. 
    Kuna mtindo uliozuka katikati ya watu wa Mungu, wa kuifanya biblia kuwa kama duka. Wanafungua biblia, wanachagua mistari wanayotaka na ahadi wanazotaka, wanaondoka nazo, huku wakiiacha mistari mingine kwenye biblia. 

    Lakini wanapoitumia hiyo mistari ya ahadi wanazotaka, na kuona hakuna matokeo yoyote, wanaona kama kwamba neno la Mungu limepungua nguvu.Hiyo si kweli. Neno la Mungu halijapungua nguvu zake wala halitakujapungua nguvu zake. Neno la Mungu hudumu milele.Kwa hiyo ni vizuri kusoma na kutafakari ahadi za Mungu juu ya maombi, lakini pia ni muhimu sana kuhakikisha kuwa unafuata maagizo yote ya utumiaji wa ahadi hizo.Kwa hiyo walio wengi. Maombi yao juu ya magonjwa, ndoa zao, wokovu wa ndugu zao na kadhalika, yamefungwa kwa kutotimiza maagizo haya ya Bwana Yesu. 

    "NINYI KILA MSIMAMAPO NA KUSALI, SAMEHENI, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. Lakini kama ninyi hamsamehi, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu" (Marko 11;25, 26). 

    Maombi yako hayajibiwi mara nyingi kwa sababu ya wewe kutosamehe wengine. Kwa maneno mengine Yesu alitaka tufahamu kuwa, tusipojifunza kusamehe wengine waliotukosea, tutabaki na dhambi mbele za Mungu. 
    Maana yake nini basi? 
    Maana yake, kutokusamehe kunahesabiwa kuwa ni kosa mbele za Mungu, na ni dhambi inayotutenga na uso wa Mungu, ili tusijibiwe maombi yetu toka kwa Mungu. 
    Kutokusamehe ni uasi Dhambi ni uasi (1 Yohana 3:4) Dhambi ni kuasi maagizo ya Mungu. 

    Kama Mungu ameagiza kwa kinywa cha Kristo kuwa kabla hatujaomba lo lote, ni lazima tusamehe kwanza; inakuwaje basi, wewe unataka ujibiwe maombi yako kabla hujamsamehe mwenzako? 
    Na kwa kutokusamehe umeasi agizo la Mungu, na kufuatana na waraka wa kwanza wa Yohana 3:4umehesabiwa kuwa umetenda dhambi.Kwa hiyo unahitajiwa utubu juu ya kutokusamehe! 
    Tuna uhakika kuwa wewe unayesoma hayo umewahi kuisema 'Sala ya Bwana' iliyoandikwa katika kitabu cha Mathayo, Sura ya 6:9-15. 
    Hatujui kama unaelewa uzito wa maneno yaliyomo katika sala hiyo. Walio wengi wanaisema kwa sababu wameikariri, lakini si kwamba wameielewa maana yake. 
    Katika sala hiyo, kuna maneno yanayohusu mambo ya kusamehe: 
    "Utusamehe deni zetu (makosa yetu) kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu (walio tukosea). (Mathayo6:12) 

    Tafakari hili neno 'kama' 
    Utusamehe makosa yetu, kama sisi nasi tunavyowasamehe waliotukosea.Hii ina maana ya kwamba kipimo kile unachokipimia katika kuwasamehe wengine ndivyo na Mungu atakavyotumia kipimo hicho hicho kukusamehe wewe mambo uliyomkosea.Sasa elewa kwamba hakuna kusamehe kukubwa, wala kusamehe kudogo. Kutokusamehe ni kutokusamehe. Na kusamehe ni kusamehe. Mizani yake inapima kitu kizima, haipimi msamaha kidogo kidogo. 

    Yesu alilifafanua jambo hili aliposema:- 
    "Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msiposamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu." (Mathayo 6:14,15). 

    Je, unaweza kusamehe bila kusahau? 
    Tulipokuwa tunaongea na mama mmoja juu ya kumsamehe mume wake, ili ugonjwa wake upone, alituambia; "Mimi nilikwishamsamehe siku nyingi." 
    Tukamuuliza; "Una uhakika?" 
    Akasema, "Ndiyo, la sivyo ningekuwa nimekwishatengana naye" 
    Tukamuuliza tena: "Kuna wakati wo wote huwa unawaza kuwa isingekuwa ni watoto mliozaa naye, ungeomba talaka au ungeondoka tu? 
    Akasema; Ndiyo, tena mara nyingi." 
    Tukamwambia: "Kusamehe kwako kuko wapi wakati bado unayahesabu makosa ya mume wako, kiasi ambacho ndoa imeshikiliwa na watoto badala ya kushikiliwa na makusudi ya Mungu?" 
    Yule mama akashangaa. 

    Kuna watu wengine wanasema wamesamehe wakati, bado kuna fundo na shina la uchungu katika mioyo yao. Kwa kinywa wanasema, wamesamehe, lakini moyoni bado hawajasamehe. 
    Na kuwatambua watu wa namna hiyo ni rahisi sana. 
    Mtu huyo huyo akimkosea tena, utamsikia akilalamika akisema; 
    "Mtu huyu nilimsamehe lile kosa la kwanza, tena amerudia. Kumbe mambo yalikuwa hayajaisha, ndiyo maana hata siku fulani alisema maneno fulani, ndiyo maana hata juzi alimgombeza mtoto wangu ......" 
    Utaona mtu huyo akiyakumbuka yote mabaya ya nyuma ambayo mwenzake alimtendea. Wengine hata hudiriki kusema kuwa: "Nitamsamehe lakini sitasahau" 
    Sasa, hiyo siyo lugha ya watu wa Mungu, waliookolewa na kununuliwa kwa damu ya thamani ya Yesu Kristo. 


    Hiyo ni lugha ya watu wasiomjua Mungu, watu wa ulimwengu huu. Na Biblia inatuambia kwamba sisi siyo wa ulimwengu huu. (Yohana 17:16). 
    Weka hilo katika roho yako. Wewe si wa ulimwengu huu, kwa hiyo lugha na maneno ya ulimwengu huu hayakuhusu. Zungumza lugha ya watu watakatifu wa ufalme wa Mungu ambao ndiyo wa uzao wako. 
    Utawezaje kusema kuwa umemsamehe mwenzako wakati bado una uchungu naye moyoni mwako? Utasemaje umemsamehe wakati kila wakati unalikumbuka na kulisema kwa watu kosa alilokufanyia? 
    Utasema huko ni kusamehe ambako Mungu anataka ufanye, ili na yeye akusamehe. 
    La hasha! 
    Kusamehe bila kusahau kosa ulilokosewa ni kusamehe kusikokamilika wala kukubaliwa mbele za Mungu. Kusema umesamehe huku bado una uchungu moyoni mwako, ni unafiki ulio wazi mbele ya Mungu. 

    Je! hujawahi kusoma mistari ifuatayo: 
    "Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue; na mtu akiua, itampasa hukumu. Bali mimi nawaambieni, kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu, na mtu akimfyolea ndugu yake itampasa baraza; na mtu akimwapiza itampasa jehanamu ya moto."(Mathayo 5:21, 22) 
    Unaweza kuona jinsi Yesu Kristo alivyofananisha hasira hiyo iliyojaa moyoni mwako juu ya ndugu yako na uuaji. Na adhabu zake zinafanana.Sasa, utakuwa unajiuliza, inawezekana kwa vipi mtu kusahau mabaya aliyotendewa?Basi nakuhakikishia kuwa inawezekana kabisa! Kwa kuwa yote yanawezekana kwake aaminiye. Na imani huja kwa kusikia neno la Mungu (Warumi 10:17) Tatizo lako ni kwamba unaona kusamehe na kusahau ni vitu viwili tofauti, kwa hiyo unavitenganisha. Huwezi ukatenganisha kusamehe na kusahau. Kwa kuwa huwezi kusamehe bila kusahau; na huwezi kusahau bila kusamehe. 

    Ufanyeje basi, uweze kusamehe na kusahau ili na Mungu naye akusamehe na kusahau makosa yako? 
    Ili tuweze kufahamu namna ya kusamehe na kusahau, ni muhimu tuielewe tabia ya Mungu juu ya jambo hili.
    October 07, 2018

    MAMBO UNAYOHITAJI KUYAJUA KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI IWE VYEPESI KUFANIKIWA KIMAISHA” SEHEMU YA 2

    Bwana Yesu asifiwe!

    Jambo la 2 tunalojifunza juu ya: “Mambo unayohitaji kuyajua kuhusu ndoto unazoota ili iwe vyepesi kufanikiwa kimaisha” ni hili:

    “Ndoto ni mlango wa kiroho ndani ya mtu, unaomwingizia vitu maishani mwake kutoka vyanzo tofauti vya ndoto”

    Ndoto ambazo mtu anaota, huwa hazina vyanzo vinavyofanana. Utofauti wa vyanzo vyake, unasababisha ufuatiliaji wake usifanane pia! Ukikosea kukijua chanzo cha ndoto uliyoota, uwe na uhakika wa kukosea pia namna ya kuishughulikia!

    Kibiblia – ndoto ambazo mtu anaota, zinaweza kutokana na chanzo kimojawapo kati ya vyanzo vifuatavyo:

    1. Ndoto zinazotoka kwa Mungu:
    Biblia inasema kwenye kitabu cha Ayubu 33:14, 15 ya kuwa: “Mungu huwa anasema na mtu “mara moja”, na wakati mwingine hata mara mbili, kwa njia ya “ndoto”…usingizi mzito uwajiliapo watu”.

    Njia mojawapo ambayo mfalme Sauli alitegemea Mungu angeitumia kujibu maombi yake, ilikuwa ni njia ya “ndoto” (1 Samweli 28:6). Asingetegemea Mungu amjibu maombi yake kwa njia ya ndoto, ikiwa huko nyuma alikuwa hajawahi kuona wala kusikia Mungu akifanya hivyo.

    Na tunajulishwa ya kuwa, njia mojawapo ambayo Mungu atakuwa anaitumia kuwaongoza watu, akimtumia Roho Mtakatifu, ni kwa njia ya “ndoto” (Matendo ya Mitume 2:17).

    2. Ndoto zinazotoka kwa shetani:
    Ndoto hii inayotajwa katika Kumbukumbu ya Torati 13:1 – 4, ni wazi kwamba chanzo chake ni “shetani”. Hii ni kwa sababu maelekezo ya ndoto hiyo, ni kutaka mtu aache kumwabudu Mungu, na badala yake afuate miungu mingine. Hii inatudhihirishia ya kuwa, shetani anaweza akaingiza kitu ndani ya mtu, kwa kutumia njia ya ndoto.

    3. Ndoto zinazotokana na mtu kuwa na shughuli nyingi:
    Tunalijua hili kwa sababu ya kile tukisomacho kwenye kitabu cha Mhubiri 5:3 ya kuwa: “…ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi….!
    Ndoto za namna hii zinaweza kumjia mtu, kwa sababu ya kujikuta amefanya “shughuli” zingine, ambazo hazipo kwenye ratiba ya Mungu – kwa ajili yake siku hiyo!

    4. Ndoto zinazotokana na hali ya kiroho ya mahali ambapo mtu amelala:
    Ndoto inayokuja kwa namna hii, tunaiona tunaposoma kitabu cha Mwanzo 28:10 – 17. Yakobo aliota ndoto ile, kwa sababu ya hali ya Kiroho ya ardhi ya eneo alilolala usiku ule!
    Ndoto ile ilimpa ufahamu Yakobo kujua hali ya kiroho ya eneo lile, na ya ardhi ile. Ndiyo maana alisema: “Kweli Bwana yupo mahali hapa, wala mimi sikujua….hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni” (Mwanzo 28:16,17).

    Utofauti huu wa vyanzo vya ndoto ambazo mtu anaweza kuota, unanisukuma moyoni kukushauri na kukuhimiza kujiombea mambo yafuatayo:

    Jambo la 1: Jiombee ili Mungu akupe kujua chanzo cha ndoto unazoota ni kipi. Soma Danieli 2:27, 28.

    Jambo la 2: Jiombee ili Mungu akiamua kukusemesha kwa njia ya ndoto, upate kusikia na kuelewa ujumbe uliomo ndani yake. Soma Ayubu 33:14, 15.


    Jambo la 3: Jiombee na “kuziba” kwa kutumia damu ya Yesu, lango la ndoto ndani yako, ili lisipitishe ndoto za shetani kuja kwako. Kumbuka Mungu aliwaambia wana wa Israeli wanaweza kutumia “damu” kumzuia Shetani asipite kwenye “milango” yao. Soma Kutoka 12:21 – 23 


    October 07, 2018

    MAMBO UNAYOHITAJI KUYAJUA KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI IWE VYEPESI KUFANIKIWA KIMAISHA”. SEHEMU 1

    “MAMBO UNAYOHITAJI KUYAJUA KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI IWE VYEPESI KUFANIKIWA KIMAISHA”. SEHEMU 1"

      Bwana Yesu asifiwe milele!

      Leo nataka nianze kukufundisha juu ya: “Mambo unayohitaji kuyajua kuhusu ndoto unazoota ili iwe vyepesi kufanikiwa kimaisha”.

      Jambo la 1: “Usiipuuzie ndoto uliyoota hata ikiwa hukijui chanzo cha ndoto hiyo!”
      Mfano wa Kwanza: Unaposoma kitabu cha Mwanzo 41:1 – 7, unaona ndoto mbili alizoota Farao, kwa usiku mmoja, na kwa kufuatana. Ndoto zile mbili zilikuwa na tafsiri moja iliyofanana. Na zilikuwa na ujumbe mmoja uliofanana, uliokuwa unamjulisha ujio wa njaa nchini Misri miaka 7 baadaye – tokea wakati ule alipoota zile ndoto.

      Farao alipoamka alijisemea moyoni mwake ya kuwa: “Kumbe ni ndoto tu” (Mwanzo 41:7). Hii ikiwa na maana ya kwamba wazo la kwanza lililomjia moyoni mwake, baada ya kuamka usiku ule, ni kuzipuuzia zile ndoto – na wala asiwe na mpango wa kuzifuatilia.

      Lakini biblia inasema, “asubuhi roho yake ikafadhaika” (Mwanzo 41:8); ikiwa ni kiashiria chenye ujumbe toka kwa Roho Mtakatifu, kwamba asizipuuzie ndoto zile! Asante Yesu hakuzipuuzia, na akatafuta msaada, ili ajue tafsiri yake. Yusufu alimtafsiria zile ndoto na kumpa maelekezo yaliyoambatana na ndoto zile. Na Farao akatekeleza maelekezo aliyopewa. Na hata njaa ilipotokea miaka 7 baadaye haikuwasumbua – kwa kuwa ujumbe wa ndoto uliwapa kujiandaa.

      Je, umewahi kujiuliza ingekuwaje kama Farao angezipuuzia zile ndoto? Ni dhahiri ya kwamba angezipuuzia – angeona tu baada ya miaka saba njaa kali yenye kudumu miaka saba – huku hajajiandaa nayo!Na kwa vile njaa ile ilikuwa ni ya “dunia yote” (Mwanzo 41:56,57), ina maana dunia yote ingekumbwa na njaa, kwa sababu tu ya Farao kuzipuuzia ndoto – ikiwa angeamua kuzipuuzia zile ndoto!

      Mfano wa pili: Danieli 4:1 – 34 tunaelezwa madhara yaliyompata mfalme Nebukadreza, kwa sababu aliipuuzia ndoto aliyoota!
      Ndoto ile – ilikuwa inampa onyo mfalme Nebukadreza, juu ya mwenendo wake aliokuwa nao wakati ule. Na ndoto ile ilimpa pia kujua adhabu atakayopewa asipobadili mwenendo wake. 
      Lakini pia kwenye ndoto ile aliyoota, alipewa maelekezo ya mambo ya kufanya, ili aliyoyaona kwenye ndoto yasimpate – lakini alipuuzia! Soma Danieli 4:27. Tena – alipewa miezi 12 ya kujirekebisha – lakini alipuuzia – na wala hakuitumia nafasi hiyo – na matokeo yake yote aliyoyaona kwenye ndoto, yalimtokea katika maisha yake!Kwa kuipuuzia ile ndoto, Mfalme Nebukadreza aliingia kwenye adhabu ya maisha yake, na afya yake kuvurugika kwa nyakati saba au miaka 7! Na pia “nafasi” yake ilikosa uongozi kwa miaka 7!

      Mfano wa tatu: Yusufu – yule aliyekuwa mume wa Mariamu, na mlezi wa Yesu wakati akiwa mtoto, aliota ndoto nne, ambazo angezipuuzia – historia ya ukristo isingekuwa ilivyo sasa!

      Ndoto ya kwanza iliyoandikwa kwenye Mathayo 1:18 – 24 tunaona akihimizwa na “malaika wa Bwana”, kuwa asihofu kumchukua Mariamu akiwa na mimba. Na akajulishwa juu ya jina na kazi ya mtoto atakayezaliwa. Biblia inasema: “Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwagiza;akamchukua mkewe” (Mathayo 1:24).

      Ndoto ya pili iliyoandikwa kwenye Mathayo 2:13 – 18, Yusufu alionywa na Malaika wa Bwana, juu ya mipango ya mfalme Herode ya kutaka kumwua Yesu. Na akaelekezwa amchukue Yesu na mama yake awapeleke Misri – na akae kule Misri hadi malaika wa Bwana atakapompa maelekezo mengine!

      Biblia inasema juu ya Yusufu baada ya kuota ndoto hiyo ya pili ya kuwa: “Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake usiku, akaenda zake Misri” (Mathayo 2:14). Hata Herode alipotuma watu Bethlehemu kumtafuta Yesu na kumuua – wakakuta hayupo! Na kwa hasira aliua watoto wote wa kiume wa eneo lile; “tangu wenye miaka miwili na waliopungua” (Mathayo 2:16).

      Ndoto ya tatu aliyoota Yusufu, iliyoandikwa katika Mathayo 2:19 – 21, ndiyo iliyomfanya aondoke Misri na familia yake, na kuanza kurudi nchini Israeli.
      Ndoto ya nne aliyoota Yusufu, iliyoandikwa katika Mathayo 2:22 – 23, ndiyo iliyomfanya amchukue Yesu na mama yake, na kuwapeleka kuishi nao “katika mji ulioitwa Nazareti; ili litimie neno lililonenwa na manabii, Ataitwa Mnazarayo” (Mathayo 2:23).

      Huo ulikuwa ni utii wa hali ya juu sana kwa Yusufu! Hasa tukichukulia maanani ya kuwa Yesu hakuwa mtoto wake wa kumzaa; tena – maelezo ya kumtunza Yesu na hata kumwepusha na hatari zilizomkabili, alikuwa anapewa kwa njia ya ndoto – ambazo watu wengi wangeweza kuzipuuzia.

      Lakini Yusufu hakuzipuuzia zile ndoto, na utii ule uliweka mwanzo mzuri wa Yesu, katika kumwandaa kwenye huduma, na kazi ya Mungu, aliyotumwa kuifanya duniani!
      Je, wewe una kiwango gani cha utii kwa maelekezo ambayo Mungu anakuletea kwenye ndoto? Au kila ndoto unaipuuzia kama mfalme Nebukadreza? Je, unaweza ukapewa taarifa na Mungu kwa njia ya ndoto ukaielewa na kuitii?

      Mtu mmoja aliyenisikiliza kwa njia ya redio tarehe 6 Nov, 2015, nikifundisha juu ya ndoto kwa kutumia biblia, alinitumia ujumbe ufuatao kwa njia ya simu:
      “Bwana Yesu asifiwe – mwalimu! Mafundisho uliyotupa leo yamegusa maisha yangu, kwa sababu kuna ndoto niliota tarehe 24.12.2013 – sitaisahau siku hii! Niliota niko kijijini kwetu huko….napambana na nyoka. Huyo nyoka alikuwa amesimama usawa wangu – na akawa ananitishia kuning’ata. Na mimi nilikuwa namkemea kwa jina la Yesu. Lakini ghafla nikaona amenigonga, na kuniuma kwenye kidole cha pili cha mguu.

      Ghafla nikashtuka toka usingizini. Nikakuta kidole kile alichonigonga na kuniuma yule nyoka katika ndoto, kinatoka damu na kinauma sana! Kulipokucha nikaenda kanisani kwetu, ambako siku hiyo kulikuwa na maombi ya kufunga. Mchungaji akawa anaombea wagonjwa. Akaniuliza unaumwa nini? Nikamjibu hivi: nimeota ndoto usiku …na kabla sijamaliza kujieleza nikaanguka.

      Kuja kushtuka na kuamka, nikaambiwa nilikuwa na pepo mauti, ambaye waliweza kumkemea, na akaondoka toka mwilini mwangu.
      Lakini tangu hapo maisha yangu yakayumba sana. Ijapokuwa nimeokoka…lakini sisongi mbele! Maisha yamekuwa magumu sana, na uchumi wangu umeyumba!Tena tangu siku hiyo niliyoota ndoto hii nilifukuzwa kwenye nyumba niliyokuwa nimepanga.Nikapanga nyumba nyingine – nayo pia tumefukuzwa mwezi wa sita mwaka huu”.

      Huo ni ujumbe nilioandikiwa na mmoja wa wasikilizaji wa mafundisho yetu. Ni dhahiri ya kwamba maombi aliyopata yalimfungua kwa sehemu fulani, na kuna sehemu alikuwa bado hajafunguliwa!



      Usiache kufuatilia somo hili kila wiki hapa hapa. Mungu aendelee kukubariki sana!
      October 07, 2018

      SOMO:NAMNA YA KUOMBEA HALI YA KIROHO YA ARDHI ILI UFANIKIWE KIMAISHA. (4&5)

      SOMO:NAMNA YA KUOMBEA HALI YA KIROHO YA ARDHI ILI UFANIKIWE KIMAISHA. (4&5)

      4. SIKU YA NNE YA SEMINA YA NENO LA MUNGU-IRINGA NA MWL CHRISTOPHER MWAKASEGE(MANA MINISTRY)

      LENGO:Kujifunza mbinu za kuomba ili hali ya kiroho ya ardhi iliyokwamisha mafanikio yako iondoke ili uweze fanikiwa.

      HATUA ZA KUMSAIDIA MTU ILI AONDOKE AU WEWE UONDOKE KATIKA HALI HIYO ILIYOKWAMISHA KUANZA UJENZI,KUENDELEA AU KUMALIZIA UJENZI..

      5.MUULIZE ALYEHITAJI KUOMBEWA IKIWA AMEWAHI KUTAFUTA KUPATANISHWA KIROHO AU KUFUATA MASHARTI YALIYOPO KTK ARDHI ANAYOJENGA AU ALIYOKWISHA JENGA.

      2FALME 17″24-29.

      Ile kwamba mwenye kiwanja amekuuzia haina maana mungu wake ameondoka pia.Unapohamia mahali hapo au kujenga hapounakutana  na masharti tofauti na mungu wako , ni lazima ufuate masharti ya pale ili uweze kukaakwa AMANI.

      Unafika eneo la kazi wanakwambia ni lazima upatane ana mungu wa pale ili ufanye kazi kwa amani.Unaweka hirizi au unasimika nyumba kwa mizimu ya mababukwababu unaamini kwa miungu ile ina umuliki wa ardhi,kumbuka Mungu ana wivu na palipo na wivu pana ugomvi, kwa hiyo Mungu hataki mtu anaye changanya mambo,hirizi penye kujenga halafu unaenda kumwomba Mungu kanisani-unaleta matatizo.Inawezekana unakabidhiwa mahali hapo haujui kuwa mahali hapo watu walikabidhi kwa miungu wao.

      6.OMBA TOBA KWA MUNGU KWA AJILI YA MAENEO YAFUATAYO:

      A.Kwa kuvunja kwa kutofuata masharti ya Mungu yanayohusu ardhi inayotumika kujenga(kuchanganya miungu).Mungu alipokuwa ana waadhibu wana wa Israeli alikuwa hana shida na watu bali madhabahu ya miungu mingine.
      B.Omba toba kwa kilichosababisha shetani akapata nafasi ya kumiliki eneo na kupata nafasi.Shetani hakupewa nchi wala mbingu wala ardhi BALI nchi walipewa wanadamu.Danieli 9:16

      Maombolezo 5:7.
      Unatubu dhambi kwa ajili yako bali uovu kwa ajili ya babu zako.

      MALAKI 1:3-4. MWANAZO 36:40-43.
      Babu yake alipojenga pamebolewa,pakabolewa lakini ameshindwa kujenga mtoto anasema watajenga lakini Mungu anasema atabomoa.
      Baba amekufa unataka kujenga hujajua nini kilichosababisha pakabomolewa unajenga!Mungu anabomoa,bila toba EDONI hawezi jenga, Mungu amezuia Edoni asijenge si kwa ajili ya uovu wa baba yake, bali uovu hutuwekea mipaka na babu zetu.

      7.OMBA MUNGU AONDOE MAZINGIRA YA UKIWA ILI ZUIO LA KUJENGA LIONDOKE NA MADHARA YAKE KWAKO AU KWA HUYO UNAYEMUOMBEA, MADHARA YALIYOZUIA UJENZI.
      EZEKIELI 35:9.

      Ukiwa unaondoa watu kutokuishi au kujenga.
      ISAYA 5:9.
      Ukiwa unazuia mipaka na wapangaji na wenye eneo.Watu wanakuwa hawaji hata kupanga hapo au kujenga.
      EZEKIELI 33:28.
      2 SAMWELI.13:20
      Ukiwa unakuhalalishia kukaa ndani hata kama unaweza fanya kazi.Ukiwa unazuia ujenzi.
      AMOSI 6:11.YEREMIA 51:26,29 15:8.
      Ukiwa unahalalisha nyumba kukomea kwenye misingi. UKIWA ni matokeo ya KUKOSA .
      8.VUNJA NA ONDOA LAANA ILIYOPO KTK ARDHI YA ENEO LA UJENZI. YOSHUA 6:26.
      Shughulika na laana iliyopo katika eneo hilo kwa Damu ya Yesu maana inasafisha kila kitu.
      9.KEMEA ILI VIONDOKE VYOTE VILIVYOKAA KTK ENEO LOTE UNALOLIOMBEA LILILOSHINDIKANA KUJENGWA AU HALIKALIKI HATA BAADA YA UJENZI. ISAYA 13:19-22.

      Ukiwa pia unapoteza wale waliobaki uwezo wa kufanya kazi kupotea.Nyumba zilizobaki tupu huwa makazi ya bundi,panya, majini na mapepo. Unaweza ukanunua gofu ukajua lipo tupu tu, au nyumba ukajua ipo tupu,au kiwanja na kama haujakemea vitu visivyo vya Mungu humo ndani vitakutesa sana, unapaswa kukemea viondke na uingie na DAMU YA YESU.

      10.OMBA MUNGU AKUJULISHE IKIWA UKIWA UMEONDOLEWA NA WATU HAO WABAYA..

      UKIWA ni ZUIO linalotumika kuzuia kitu flani kwa ajili ya mtu yule aliyewekewa kutengeneza EZEKIELI 45:1-4, 48:8-9.

      Kuna majengo mengi yamekwama kwasababu yamewekewa ZUIO,kama Mtumishi wa Mungu unatakiwa uondoe zuio hilo.

      YEREMIA 4:27-28. ISAYA 6:1-4.
      Roho Mtakatifu akishuka atakupa FURAHA badala ya MAOMBOLEZO.Watu wengi wana magari lakini hawana nyumba kwasababu ya zuio ktk ulimwengu wa roho kuwa na UKIWA washindwe kujenga,
      11.WEKA WAKAFU KWA MUNGU HILO ENEO.
      MkabidhiMungu hilo eneo, inawezekana Mungu amekupa eneo lakini anataka umkabidhi kwake rasmi.Ukilishikilia na kulimiliki eneo hilo kwa Damu ya Yesu Mungu anakupa plan ya hilo eneo.Weka wakfu ardhi,mipaka,misingi,malango na ramani ya kiwanja.
      Mungu hukupa vipimo, vitakuwa vyumba vya watoto wangapi, wageni wa namna gani?.Mungu akupe cha kwako usiige cha wengine bali pata cha Mungu maana ana plan ya maisha yako ya baadaye.Weka wakfu kwa kila kitu maana kwenye ramani zingine kuna vitu visvyo vya Mungu pia.

      12. VISEMESHE ARDHI NA MBINGU VISIKWAMISHE UENDELEZAJI WA UJENZI NA UTUMIAJI WA KITAKACHOJENGWA.KUMBUKUMBU LA TORATI 32:1.

      Ni vizuri kuitangazia ardhi kilichoondoka na Mungu amenipa eneo hili ili usikwamishe.Ukishasemesha ardhi inasikia na mbingu inasikia. Neno linaposema mbingu iliwafunika maana yake ni kwa ajili ya watu wengi bali inaposema mbingu ikikufunikia ina maanisha ni kwa ajili ya mtu mmoja

      5. SIKU YA TANO NA YA MWISHO

      LENGO:Kujifunza mbinu za kuomba ili hali ya kiroho ya ardhi iliyokwamisha mafanikio yako iondoke ili uweze fanikiwa.

      MBINU ZA KUOMBA ILI KUWAFUNGUA WALIOFUNGWA NA JELA YA KIROHO YA ARDHI Matendo 16:26.

      Tunajifunza Paulo alikemea lile pepo lakini kumbe ulikuwa mradi wa watu wa pepo wa uaguzi,unaweza ukawa unafanya vitu kumbe watu wengine ni mradi wao na ukaanza kuapata vita toka kwao(waganga)
      Paulo alipofanya maombi kule gerezani tetemeko halikutetemesha gereza tu bali MISINGI ya gereza ilitikisika na milango ikafunguka.
      Mstari 26-milango ya gereza ilifunguliwa kabla vifungo havijalegezwa, vigungo hulegezwa na matokeo ya msingi na milango kulegezwa.
      Ile nguvu ilienda kwenye misingi ya KIROHO  iliyofunga akina Paulo wasiendelee kwa jinsi ya mwili pia.Jinsi ya kiroho  haimtishi shetani bali misingi ya kiroho, tunatembelea madaha kwa Kristo kwasababu tumekombolewa KIHALALI kwa Damu yake.Ni Lazima kuombea misingi ya kroho ya mahali hapo ili milango ya mafanikio ifunguke na iachie.
      MAOMBOLEZO 3:33-35.
      Inaonyesha watu wote walifungwa kwenye ardhi,unaweza kuwa unatembea kwa madaha uko huru  mtaani lakini kumbe kiroho ni mfungwa wa ardhi hiyo na hufanikiwi.
      Kumbukumbu la Torati 6:12 7:8
      Nchi inaweza kuwa imewekewa utumwa kwenye ardhi lakini watu wakawa wanaishi hivyo wakifikiri wapo huru kumbe kuna mahali wamefungwa wasiendelee.
      ISAYA 14:24-27.
      Ukikanyaga ardhi  kwa mamlaka aliyokupa Mungu ndipo NIRA yako itakapoondoka kwa kifungo kilichokufunga. Ukikanyaga juu ya ardhi ile nira itaondoka  na kubatilisha ardhi ktk ulimwengu wa kiroho.
      KIFUNGO CHA KIAPO KATIKA ARDHI.
      WAEBRANIA 3:14-19 HESABU 14:22-45.
      Neno la Mungu linaposema “KAMA NIISHIVYO” maana yake ni KIAPO CHA MUNGU.
      Mungu alifunga kiapo kwa wana wa Israeli jangwani walishindwa fanikiwa kwasababu ya uasi,
      HESABU 30:2, 12-16.
      Kiapo ni kifungo cha kiroho.Nafsi inabeba hisia,maamuzi,fikra, nia na makusudi ya mtu.
      Ikiwa umefungwa katika kiapo flani NI LAZIMA ukibatilishe kile kiapo na UTENGUE.
      EZEKIELI 21:18-23.
      Kwenye mistari hii inaposema alipelekwa kwenye NJIAPANDA ili ale kiapo ,NJIAPANDA maana yake ni KUKOSA MAAMUZI, unakuwa njiapanda uolewe au usiolewe,usome au usisome,ujenge au usijenge,ufanye huduma ya Mungu au kazi nyingine,biashara au siasa n.k UPO NJIAPANDA.
      Unaweza ukaota ndoto vitu vikatokea ndotoni -ardhi imefungwa ufeli,inakufunga usifanikiwe kwa njia za KI-MUNGU kabisa bali ufanikiwe kwa njia za ki-miungu hiyo unakuwa umefungwa usipotangua itakutesa.
      Mji wa Yeriko ulikuwa umefungwa jela ya kiroho ya ardhi.Mungu alipokuwa amepeleka watumishi wake alikuwa hana shida na Yeriko bali shida yake ilikuwa kwa Rahabu ktk ukoo wa Yesse kwasababu ardhi ilimfunga.
      Watakuja wahubiri atahubiri watu hutapona kumbe tatizo liko kwenye ardhi ambayo ndiyo imekufunga katika tatizo hilo.
      Punda wa Yesu alikuwa amefungwa kinabii kwa ajili ya BWANA YESU na hakuna aliyemtumia mpaka Yesu alipokuja.Unaweza pia nawe katika familia,ukoo,jamii, au taifa lako umekuwa punda uliyenenewa na mababu zako imefika kipindi chako cha ujana ustawi unashindwa! kwasababu umefungwa ktk kiapo flani katika familia au ukoo hausogei ktk Elimu, au biashara, au kiuongozi, ndoa,kiuchumi,kiroho,,kujenga,au n.k.PUNDA UMEFUNGWA.

      Na ivyo hivyo Mungu alisema  kwa ajili ya maisha yako atafanya CHAKE.imefika unataka ufanye kingine unachotaka wewe HAKITAENDA bali BWANA atafanya chake kwasababu BWANA anasema ana haja nawe, utafanikiwa na kustawi ni kwasababu  cha BWANA( kwasababu maisha yako yamefungwa kumtumikia Mungu)

      Ni lazima ukae kwenye LANGO kwasababu Mungu anataka kukupitisha  ili kufungua milango ya mafanikio yako ili ufike kule BWANA alipoweka KUSUDI LAKE na kwa KIWANGO CHAKE sio viwango vya wanadamu.

      ILI KUFUNGULIWA TOBA NI MUHIMU kwasababu 1.Mungu anakusamehe na 2.Mungu atakurehemu na DAMU YA YESU itasema maneno mazuri juu yako, UTAMILIKI juu ya VYOTE  na ROHO WA BWANA atakuwa Juu yako.
      Mwisho wa Semina hii, tutendee kazi haya tutafanikiwa,tusiwe wasikilizaji tu.

      HAKIKA TUTABARIKIWA NA KULA MEMA YA NCHI.


      October 07, 2018

      SOMO:NAMNA YA KUOMBEA HALI YA KIROHO YA ARDHI ILI UFANIKIWE KIMAISHA (2&3)

      SOMO:NAMNA YA KUOMBEA HALI YA KIROHO YA ARDHI ILI UFANIKIWE KIMAISHA (2&3)


      LENGO: Kujifunza mbinu za kuomba ili hali ya kiroho ya ardhi iliyokwamisha mafanikio yako iondoke ili uweze fanikiwa.
      HATUA  ZA KUFANYA ILI UONDOKE HAPAO ULIPO AU UMWOMBEE MTU ALIYEKUJA KUOMBA MSAADA UMSAIDIE KUTOKA HAPO.

      1.PELEKA OMBI HILO KWA MUNGU.Usijaribu kumsaidia huyo mtu au kujisaidia bila kumuuliza Mungu kwasababu wewe huna jibu la matatizo  yake bali kwasababu una mahusiano mazuri na Mungu na pale anapotaka maombi yake. ZABURI 107:19-20.Wana wa Israeli walipoenda kinyume na Mungu walimlilia Musa na yeye pia akamlilia 
      Mungu.

      2.POKEA NENO LA MUNGU UNALOPEWA NA MUNGU KWA AJILI YA HUYO ALIYEKUOMBA UMWOMBEE AU UJIOMBEE.ZABURI 107:17-20.

      Unajiuliza unafanyaje? Mungu anakuletea NENO ISAYA 55:11.Ukitaka kufanikiwa kwa mpango wa Mungu lazima upokee NENO. YEREMIA anasema Neno la Bwana likanijia likasema. Kwa hiyo ni lazima usikie Neno la Bwana sio lako.

      3.OMBA MUNGU AKUPE KUSIKIA MUONGOZO WAKE KWAKO KUTOKA KWENYE NENO ULILOPEWA. RUMI 10:17.

      Imani huja kwa kusikia.Lazima ujue utaratibu Mungu alionao katika kukufanikisha.Imani chanzo chake ni kusikia kwa NENO LA KRISTO.
      Mungu anaweza sema na wewe kupitia mistari iliyopo kichwani mwako,kusoma Biblia,CD,kipindi cha redio au Runinga ambako huwa kuna Neno ameliweka huko ili upate sikia ujumbe wake.
      Ni lazima uchimbe historia ya huyo mtu au ikiwa ni wewe ili kufuatilia hiyo hali anayolalamikia kutokufanikiwa kwake au hali inayofanya kutokufanikiwa kwako.2FALME 24:1,8-10 23:36-37.Mungu atakupa maarifa jinsi ya kujihudumia wewe au mwingine.Umejua ni adhabu ya ukoo wapi ni lango ya dhambi hiyo.Wakiendelea kukalia KITI cha DAUDI adhabu itaendelea kukufuata inabidi usikae ili utoke.Kama kuna Kiti cha ukoo,familia,taifa umekalia usipotoka hapo atakuja mwingine mwisho utarudi pale pale au utatenda yale yale.
      Yehoyakimu alikaa miezi 3 akaondolewa na baada ya miaka 3 akaasi akawa chini Nebukadreza(Shetani).

      4.OMBA TOBA KWA AJILI YA DHAMBI  ZA MAOMBI ALIYOLETA YULE MTU AU YAKO KWASABABU YA UOVU WA WAZAZI AU WATANGULIZI ULIVYOSABABISHA WASIFUATE MAAGIZO YA MUNGU.YEREMIA 22:21.

      Sio kutubu tu bali kujua mahali dhambi ilipoingia(ujana wa wazazi wao au wako),mlango wa kutokumsikia Mungu DANIELI 6:19.KUTOKA 20:5.
      Mungu hapatilizi dhambi bali uovu.Kuna tofauti kati ya DHAMBI na UOVU.DHAMBI ni uasi-kwenda kinyume na maagizo ya Mungu(unatumia vitu kinyume na alivyokuagiza).UOVU ni udhaifu.
      Tunatubu kwa ajili ya dhambi zetu na uovu wa babu zetu.Unaweza kwenda jela kwasababu hakukuwapo mtu wa kutetea kisheria katika lile kosa na si kwasabau umetenda dhambi.Dhambi maana yake unatumia vitu ulivyopewa kinyume na utaratibu.Mungu hapatilizi dhambi bali udhaifu,ule udhaifu unaacha kukusaidia.Wote tumetenda dhambi na kukosa utukufu wa Mungu.Udhaifu ni hali inayokaa kwenye mwili,nafsi,roho na kujenga mazingira uzao wako uliotoka kwa babu au baba.Huzaliwi na dhambi ya kunywa pombe bali udhaifu, huwezi stahimili hali hiyo,ukisikia harufu ya pombe huwezi stahimili.Kwanini utubu dhambi? ili Mungu aingilie kati ili uasi usiendelee.Mungu aingilie kati uovu, ili udhaifu huo usiendelee kwa watoto wako.Ni lazima ufute kisheria ili utoke hapo.

      5.          FUTA AU ONDOA LAANA KATIKA ARDHI KWA KUTUMIA DAMU YA YESU.
      YREMIA 22:29-30.

      Ardhi imeandika na kutunza kumbukumbu. WAEBRANIA 9:19-24.
      Damu ya YESU inaondoa na kufuta dhambi.Damu ya Yesu inaonekana kwa ajili ya mtu unayemuombea au wewe na kutaka kumsaidia.Mbinguni kuna nakala mbili.!.Nakala za makosa yako mbinguni 2.Nakala za mashtaka ya shetani kwa Mungu.
      Damu ya Yesu inakuja kufuta mashtaka yote lakini kwenye ardhi yapo.Unasema nafuta maneno yote ktk ardhi yanayofanya nisifanikiwe.Ardhi imetumika kama polisi na magereza maana kesi haiwezi kwenda mahakamani kama nakala ya kesi haipo.Ardhi imeiumbiwa ikuzie kama hati,ardhi itakapoona Damu imekuja na Jina la Yesu itafuta mashitaka yote.Nebukadreza alipata nguvu toka ardhi kuwatesa wana-Israeli.

      6.LAZIMA UKEMEE ROHO AMBAYO INAYOZUIA MAFANIKIO.
      Kemea mzaingira ya uasi,kemea roho ya UKIWA kwasababu unaishi kama umenyang’anywa kitu(Mume,kazi,mke,uchumi,gari,biashara n.k)Kazi ya roho ya ukiwa ni kukunyang’anya uwe mikiwa,uwe na hali ya upweke.KOLOSAI 1:13-14.
      Yesu anaachilia Damu na kukumboa na anaachilia hati ya kukumboa kutoka hali hiyo.

      7.MWOMBEE HUYO MTU AU JIOMBEE WOKOVU NA UTII KWA MAAGIZO KWA MUNGU ATAKAYOKUWA ANAMPA/ANAKUPA NA AGANO LAKE. YEREMIA 22:29.
      Maombi hayakufanikishi bali NENO toka kwa Mungu(sio kuendeda kila mkutano ukaombewe tu bali uwe unaomba Mungu akupe Neno toka kwake la kukukusaidia).
      Ukitaka mafanikio Mungu anakupa Neno ili uwe msikivu kwa kukupa mawazo ili usikwame.

      8.OMBA MUNGU AKUONDOLEE HALI YA UKIWA KATIKA NYUMBA YAO AU YAKO ARUDISHE KITU KITAKACHOKUONDOLEA UKIWA.

      Dunia ilipokuwa ukiwa kuna kitu Mungu alikirudisha.Akikuondoa kwenye NAFASI huacha hali ya ukiwa.Habili alipouwawa hali ya ukiwa iliingia kwenye familia ya Adamu,vizazi saba mpaka Seth alipozaliwa alirejesha hali ya faraja kwasabu kuna kitu Adamu alikuwa amekosa Seth alikirejesha(Kumcha Bwana)
      Mfao kwenye familia atakapopatikana mtu mmoja awe mtoto,mjukuu au kilembwe ambaye amebeba kitu flani cha wazazi ambacho wanakipenda iwe biashara,uchaji wa Mungu,uongozi n.k faraja hurejea katika familia Yeremeia 22:5

      9.ISEMESHE ARDHI NA MBINGU KWA UPYA VISIKWAMISHE MAFANIKIO YAKO AU YAKE.KUMB LA TORATI 31:28-30, 30:19-20 32:1.
      Unafanya hivyo ili ardhi na mbingu zitunze kumbukumbu na maneno utakayosema ili baadaye pasiwepo na cha kukukwamisha/kumkwamisha mafanikio yako/yake.



      SEHEMU YA TATU (3)

      LENGO:Kujifunza mbinu za kuomba ili hali ya kiroho ya ardhi iliyokwamisha mafanikio yako iondoke ili uweze fanikiwa.
      Ikiwa mtu amekuja kwako kuomba msaada wa maombi kwasababu hafanikiwi au wewe mwenyewe hufanikiwi ktk ujenzi unaotaka kujenga au aliokwisha anza kujenga au umekwama mahali unataka kumalizia fedha zinapotea.Unamuombaje au unamuombeaje?.
      HATUA ZA KUFANYA ILI UTOKE AU ATATOKE HAPO.

      1.PELEKA OMBI HILO KWA MUNGU.
      Kwasababu jibu huna bali kwasababu ya mahusiano uliyonayo na Mungu unaye mwamini wahitaji mpeleka kwa Mungu.

      2.POKEA NENO LA MUNGU KWA AJILI YA HUYO ALIYEOMBA UMUOMBEE AU KWA AJILI YAKO.

      ZABURI 107:19-20,ISAYA 55:11.
      Neno la Mungu lina wazo na mikakati ndani yake inayotoa mvua mvua na kunyesha ili kumea NENO la kukusadia ktk kukufanikisha.
      Nchi inaweza kuwa na WAOMBAJI wazuri ila kama hawana NENO ni ngumu sana kufanikiwa.Unaomba mvua inanyesha lakini hujaandaa MBEGU ni vigumu kustawi.Ni lazima na ni sheria ya KI-MUNGU kupokea Neno ili ustawi.

      3.OMBA MUNGU AKUPE KUSIKIA MWONGOZO WAKE KWAKO KUTOKA KWENYE NENO ULILOPEWA NA MUNGU ULIPOMWOMBEA HUYO MTU AU WEWE.RUMI 10:17.

      Ni lazima usikie Sauti ya NENO ambayo hutengeneza uhakika(IMANI) ili kufungua macho ya imani kuona kila linalotarajiwa.Ebr 11:3.
      Imani huja kwa kusikia.UTasikiaje? Kwa jinsi linavyokuja.KUMB LA TORATI 8;7,11-12.Kuna suala la umiliki wa ardhi kiroho na kimwili,kabla ya umiliki wa kimwili lile eneo lilikuwa halali kiroho kwa wao.Si unajenga tu bali kiwango cha kujenga ambacho Mungu anataka.Unajenga kwa ubora upi?.unajenga na kukaa nadani yake ni lazima ujenge na kutumia 

      4.OMBA MUNGU AKUPE KUTAMBUA MASHARTI YA KIROHO YALIYOP KWENYE ARDHI INAYOJENGWA JUU YAKE AU UNAYOKUSUDIA KUJENGA.kumb 8:7,11-12.

      Katika sheria za umiliki kuna umiliki wa kiroho kwanza kabla ya umiliki wa kimwili.Sheria za umilikiwa kiroho zina nguvu kuliko za kimwili
      Endelea kutufuatilia Jifunze na Uelimike kwa Muendelezo wa Mafundisho.