IJUE BIBLIA | LISTENING GOD'S VOICE THROUGH GOSPEL SONGS


Breaking News

Showing posts with label Holy Spirit. Show all posts
Showing posts with label Holy Spirit. Show all posts

Wednesday, 7 August 2019

August 07, 2019

IJUE BIBLIA | KUNA HAJA YA KUWA NA ROHO MTAKATIFU?

IJUE BIBLIA | KNOW THE BIBLE

KUNA HAJA YA KUWA NA ROHO MTAKATIFU?



Yohana 14:26

26 Lakini yule Msaidizi, yaani Roho Mtakatifu, ambaye Baba yangu atamtuma kwenu kwa jina langu, atawafundisha mambo yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.

Tafakari ya somo hili je tunahitaji kuwa na Roho Mtakatifu?
kwa kawaida mwanadamu anapitia changamoto nyingi sana katika maisha yake. Na njia ya pekee ya kupata maarifa sahihi na kuendelea kuwa na imani na tumaini kwamba jambo hilo ama changamoto hiyo anayopitia ni ya Roho Mtakatifu.

Warumi 8:26

 '' Kadhalika ROHO naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini ROHO mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.''Kumbuka mpendwa changamoto unayopitia ni ya muda tuu.

Maarifa sahihi yanapatikana kwa kujifunza kutoka chanzo sahihi na hapa ni Roho Mtakatifu pekee ndie atoae maarifa sahihi. 
Roho Mtakatifu pekee ndie awezae kutukumbusha ahadi zile tulizopewa tokea mwanzo.

Nakutakia tafakari njema na karibu tushirikishane kwa yale unayojifunza.

Mungu wa Mbinguni akupe Roho wa ufunuo na wa Maarifa ukamjue Mungu zaidi.
August 07, 2019

IJUE BIBLIA | ROHO MTAKATIFU AKIWA JUU YAKO

IJUE BIBLIA | KNOW THE BIBLE

ROHO MTAKATIFU AKIWA JUU YAKO




Matendo ya Mitume 1:8
8 Lakini mtapokea nguvu akishawajilia Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu na Yudea yote na Samaria, hadi mwisho wa dunia.”

Tumeona habari za kumpokea Roho Mtakatifu yakuwa tutapompokea mito ya maji yalio hai yatatoka ndani ya kila aliyeamini.

leo tuangalie habari za yeye kutua juu yetu. Maandiko haya yanatueleza atakapotujilia juu yetu tutapata NGUVU na kuwa mashaidi.

Tafakari
Nguvu hiyo ni ipi?
Je Roho ameshakuja juu yako?
Na utakuwa shaidi wa nini?

Nakutakia tafakari njema na karibu tushirikishane katika comment unayojifunza na kutafakari.

Tuesday, 6 August 2019

August 06, 2019

IJUE BIBLIA | MITO YA MAJI YALIO UHAI

IJUE BIBLIA | KNOW THE BIBLE

MITO YA MAJI YALIO UHAI


Yohana 7

38 Kama Maandiko yasemavyo, ye yote aniaminiye, vijito vya maji yaletayo uzima vitatiririka kutoka moyoni mwake.”
39 Yesu alisema haya kuhusu Roho Mtakatifu ambaye wote waliomwamini Yesu wangempokea, kwani mpaka wakati huo, Roho alikuwa bado hajatolewa, kwa kuwa Yesu alikuwa bado hajainuliwa na kutukuzwa.

Tunapoanza anza mwez huu wa 8 tupate tafakari juu ya Roho Mtakatifu.
Tunajifunza katika maandiko juu ya MITO YA MAJI YALIO UHAI YATATOKA NDANI YA KILA MMOJA ALIYE AMINI.

Je mimi na wewe tumeamini?
Je Mito hii ya uhai tunaijua?
Na je mito hii ya uhai imetiririka kwa waaminio?

Katika tafakari Roho wa Mungu akupe Hekima na uelewa na Mito ya uhai ikaachiliwe ndani yako mwezi huu.