IJUE BIBLIA | LISTENING GOD'S VOICE THROUGH GOSPEL SONGS


Breaking News

Showing posts with label God. Show all posts
Showing posts with label God. Show all posts

Wednesday, 7 August 2019

August 07, 2019

Life Lessons you need to learn about Heaven Kingdom

IJUE BIBLIA | KNOW THE BIBLE


UFALME WA MUNGU



Warumi 14:17 Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

17 Kwa maana Ufalme wa Mungu si kula na kunywa bali ni haki, amani na furaha ndani ya Roho Mtakatifu.


Tafakari juu ya huu ufalme ambapo maandiko yanasema tutaingia na SIO KWENDA. Hakuna kwenda kwenye ufalme bali kuna kuingia. hivyo hakuna safari yoyote tutayofunga na kusafiri kwenda huko ila tunaingia kwakua Ufalme huo upo tayari ndani ya kila mmoja, na Ufalme huo sio wa kula na kunywa kwa maana nyingine ni Roho ya mtu ambayo ni sura na mfano wa Mungu ambao ndani yake huangaza Haki, amani na furaha ambayo roho hii inaishi ikiwa hapa duniani katika mwili pamoja na yule Roho wa Mungu yaani Mtakatifu.
Tafakari njema na karibu kushirikiana nasi katika tafakari hizi.

Mungu wa akutie nguvu katika kujifunza mambo ya Ufalme wa Mungu, mamlaka yake na ukuu wake,
Barikiwa na Bwana wetu Yesu Kristo, mpendwa
August 07, 2019

IJUE BIBLIA | KUNA HAJA YA KUWA NA ROHO MTAKATIFU?

IJUE BIBLIA | KNOW THE BIBLE

KUNA HAJA YA KUWA NA ROHO MTAKATIFU?



Yohana 14:26

26 Lakini yule Msaidizi, yaani Roho Mtakatifu, ambaye Baba yangu atamtuma kwenu kwa jina langu, atawafundisha mambo yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.

Tafakari ya somo hili je tunahitaji kuwa na Roho Mtakatifu?
kwa kawaida mwanadamu anapitia changamoto nyingi sana katika maisha yake. Na njia ya pekee ya kupata maarifa sahihi na kuendelea kuwa na imani na tumaini kwamba jambo hilo ama changamoto hiyo anayopitia ni ya Roho Mtakatifu.

Warumi 8:26

 '' Kadhalika ROHO naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini ROHO mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.''Kumbuka mpendwa changamoto unayopitia ni ya muda tuu.

Maarifa sahihi yanapatikana kwa kujifunza kutoka chanzo sahihi na hapa ni Roho Mtakatifu pekee ndie atoae maarifa sahihi. 
Roho Mtakatifu pekee ndie awezae kutukumbusha ahadi zile tulizopewa tokea mwanzo.

Nakutakia tafakari njema na karibu tushirikishane kwa yale unayojifunza.

Mungu wa Mbinguni akupe Roho wa ufunuo na wa Maarifa ukamjue Mungu zaidi.

Tuesday, 6 August 2019

August 06, 2019

IJUE BIBLIA | MITO YA MAJI YALIO UHAI

IJUE BIBLIA | KNOW THE BIBLE

MITO YA MAJI YALIO UHAI


Yohana 7

38 Kama Maandiko yasemavyo, ye yote aniaminiye, vijito vya maji yaletayo uzima vitatiririka kutoka moyoni mwake.”
39 Yesu alisema haya kuhusu Roho Mtakatifu ambaye wote waliomwamini Yesu wangempokea, kwani mpaka wakati huo, Roho alikuwa bado hajatolewa, kwa kuwa Yesu alikuwa bado hajainuliwa na kutukuzwa.

Tunapoanza anza mwez huu wa 8 tupate tafakari juu ya Roho Mtakatifu.
Tunajifunza katika maandiko juu ya MITO YA MAJI YALIO UHAI YATATOKA NDANI YA KILA MMOJA ALIYE AMINI.

Je mimi na wewe tumeamini?
Je Mito hii ya uhai tunaijua?
Na je mito hii ya uhai imetiririka kwa waaminio?

Katika tafakari Roho wa Mungu akupe Hekima na uelewa na Mito ya uhai ikaachiliwe ndani yako mwezi huu.