IJUE BIBLIA | LISTENING GOD'S VOICE THROUGH GOSPEL SONGS


Breaking News

Showing posts with label NAFASI YA VIJANA KATIKA KANISA.. Show all posts
Showing posts with label NAFASI YA VIJANA KATIKA KANISA.. Show all posts

Wednesday, 31 July 2019

July 31, 2019

IJUE BIBLIA | MAKOSA YA WATU WENGINE YASIKUFANYE NA WEWE UKOSEE

IJUE BIBLIA | KNOW THE BIBLE




MAKOSA YA WATU WENGINE YASIKUFANYE NA WEWE UKOSEE!




Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi.
Leo watu wengi wamemkosa Mungu kwa sababu ya makosa ya watu wengine. Eti kwa sababu mtu wako wa karibu kaanguka dhambini basi na wewe ndio uanguke uanguke dhambini!au ukosee eti kwa sababu na mwenzako kakosea! Nimejaribu kuliangalia jambo hili kwa ukaribu sana,na kugundua kwamba wengi wanaanguka dhambini kwa sababu ya watu wao wa karibu nao wameanguka.
Wale watu wa vyuoni wanaelewa ninazungumza nini mahali hapa. Maana wengi wao wanaanguka sana kwa sababu ya marafiki walionao karibu;hujawahi kuona mtu ni mzinzi kwa sababu tu rafiki zake ni wazinzi? Lakini leo ni lazima ujifunze kwamba hakuna haja wala sababu ya wewe mtu wa Mungu kukosea,kumkosa Mungu kwa kigezo cha makosa ya watu wengine.
“ Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu;akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake.Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao.” Mwanzo 9:20-23
Hamu mwana mdogo wa Nuhu alikosea kuuona uchi wa baba yake Nuhu. Kitendo cha kuona “tupu ya baba yake” kilikuwa ni kibaya sana,Hamu alikuwa anao uwezo wa kutokukosea hivyo! Mbaya zaidi baada ya kuuona uchi wa babaye hakuchukua hatua nzuri ya kufunika kimya kimya,bali yeye alienda kuwapasha habari nduguze juu ya tupu ya babaye!!! Kosa la Hamu lingeweza kuwafanya Shemu na Yafethi kukosea,lakini akina Shemu wakatenda hekima.
Kumbe inawezekana makosa ya watu wengine yasikufanye na wewe ukakosea. Ebu Jifunze kwa Shemu na kwa Yafethi watu ambao walitenda vyema katikati ya makosa ya mtu mwingine. Kukosea kwa Hamu kulipelekea laana kwa mtoto wake Kanaani (uzao wa Hamu ulilaaniwa,kwa kosa moja tu)hapo unaweza kuona kwa kosa la mtu mmoja anaweza kukufanya nawe ukakosa hatimaye na wewe ukaingia kwenye laana ambayo kwa kweli haikuwa yako!
Shemu na Yafethi kana kwamba walijua hatari ijayo,gafla wakaona isiwe shida-wakajitanda vazi mabegani mwao na kumfunika mzee wao aliyekuwa uchi. Jifunze sana katika eneo hili,kwamba huna sababu za kumsikiliza weee! Mtu mkosa,badala yake chukua hatua mara moja ya kusawazisha kosa hilo,au la!basi kaa mbali na story zake za muda mrefu usije ukaingizwa katika hali ya kukosa na ukapokea laana za bure. Kumbuka,leo kuna watu wamekaa mkoa wa kukufanya ukosee na kumkosa Mungu,jitahidi kuwakwepa watu hao kwa gharama yoyote ile.
Mfano; mtu wako wa karibu anakujia gafla na anakushirikisha udhaifu aliouona kwa mtumishi wa Mungu ambaye kwa huyo mtumishi ni baba au mama yako wa kiroho. Nawe bila kujua unanogewa na mastory ya kumsema mtumishi wa Mungu kwa sababu mtumishi alijisahau akakaa vibaya. Kule kuendelea kumsema,ujue nyote wawili mtaangukia kwenye laana! Ni afadhali sana ukimbie hizo story,kisha utafute namna ya kumfunika mtumishi huyo kwa maombi asiendelee na tabia au hali aliyokuwa nayo.
Leo sisi wachungaji tunaangaika sana kuwaombea watu tukidhani kwamba wamelogwa,lakini kumbe sio kulogwa,bali ni laana wanazotembea nazo kwa sababu ya tabia zao kama tabia ya Hamu. Wewe unafikiri mambo yako yakiwa hayaendi basi umelogwa tu? Hapana mambo mengine unajiloga mwenyewe kwa makosa yako kwa sababu ya wengine waliokosea. Unanipata vizuri lakini? 
Ikiwa wewe ni kijana wa kiume au wa kike ni muhimu kujifunza kuwa makini hapo nyumbani kwenu unapoishi na ndugu zako wakubwa au wadogo zako. Unapoona fulani nduguyo kaiona aibu ya baba yako kwa sababu ya ulevi wake,basi wewe kataa kushiriki mazungumzo mabaya juu ya baba yako,bali wewe tafuta ufumbuzi wa tatizo hilo,jaribu kumfunika mzee wako na wale usiendelee kushiriki mazungumzo hayo ya kuufunua aibu ya mzee wako. 
Kumbuka;hata kama mzee wako anaitwa cha pombe wala hajaokoka,lakini ujue anayo nguvu ya kukutamkia laana na hiyo laana itakupata tu kwa sababu kwanza yeye ni mzazi wako,pili hiyo laana ina sababu ya kukupata maana umeufunua utupu au aibu ya baba yako kwa njia ya maneno ya kinywa chako pamoja na nduguyo,wote wawili mtalaaniwa hata kama mmeokoka. Ni muhimu kukaa kimya,na kufanya maarifa kihekima kuficha aibu ya mzee wako.
Hamu alipouona utupu wa babaye,alilaaniwa mwanaye Kanaani kwa makundi kabisa kwa maana maumivu ya laana yasingelikuwapo kama laana zile zingeenda kwake moja kwa moja,bali mtoto alipolaaniwa maumivu ya laana yalikuwa ni makubwa sana kwa sababu kizazi chake Kanaani ndicho kilichotembea kwenye laana hiyo,maana Kanaani alikuwa mtumwa wa Shemu. 
Hakuna sababu ya kuanguka dhambini eti kwa sababu ya wengine wameanguka dhambini. Fanya hivi;ikiwa wenzako wameanguka dhambini wewe usishiriki makosa yao,zaidi sana uwe tofauti nao,washauri na uwaombee.
July 31, 2019

IJUE BIBLIA | NJIA YA HAKI

IJUE BIBLIA | KNOW THE BIBLE




NJIA YA HAKI



Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi.
Bila shaka kama ikiwapo njia ya haki basi ni dhahili njia ya uovu na yenyewe itakuwepo tu. Na kama kuna njia uovu / ubaya basi kabla ya kujua njia ya haki,ni vyema ukaijua njia ya uovu. Neno “ njia” kama linavyotumika kwenye biblia halina maana ya njia kama barabara tulizonazo ambazo tunatembelea. Kumbuka; Biblia inajaribu kusema nasi katika lugha ya picha,lugha raisi ya kibinadamu ili kusudi upate kuelewa vizuri. Hivyo,neno “ njia” ni “mfumo binafsi au taratibu binafsi“. Inawezekana ukawa ni mfumo binafsi wa maisha ya mtu,au taratibu zinazofuatwa na mtu binafsi. N.K

“Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu,Lakini mwisho wake ni njia za mauti.“Mithali 14:12
Andiko hili ni sawa na kusema “upo taratibu fulani / mfumo binafsi wa maisha ya mtu unaonekana sawa machoni pake,Lakini mwisho wa mfumo huo ni uharibifu / maangamizo/ mauti“
Ikiwapo taratibu fulani ya maisha yako uliyochagua kuishi,ujue hiyo ni njia. Lakini je ni taratibu gani uliyonayo? Bila shaka taratibu za maisha binafsi ya mwanadamu ni mbaya tu siku sote,kwa sababu mawazo yetu ni mabaya kama Mungu hajausika hapo. Katika mfumo binafsi wa maisha ya mtu mwovu siku zote hujiona yeye yupo sahihi sana kuliko anavyoonekana. Na huo ndio ukweli wenyewe!! Hujawahi kuona mtu ambaye mtenda uovu akijitetea kwamba yeye hana makosa,ila makosa anasingiziwa!! Lakini ujue mtu huyu akishupaza shingo wakati wa kuonywa ujue atavunjika na kukosa dawa ( Mithali 29:1)
“ Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.” Mathayo 7:13-14
Andiko hilo,nataka nikutazamishe neno “njia” kama lilivyotumika. Neno njia ,bado linatupa maana ile ile kwamba ni mfumo wa maisha. Kwamba mfumo wa maisha ya watu unaowaingiza watu wengi motoni ni mpana ( yaani watu wengi wapo kwenye mfumo au taratibu hizo,za maisha ya kila siku)
Lakini pia “njia” / taratibu ni ndogo,zinazowapeleka watu mbinguni ( si wengi wanaoishi kwenye taratibu sahihi za kiungu,na wengi hukosa taratibu hizo.)Watu wengi wamejikuta wakiishi maisha kama fulani aishivyo. Au watu uishi kama dunia itakavyo. Na huku ndiko kunakoleta matokeo ya mauti mwishoni.
Macho yanatabia ya kudanganya siku zote na ndio maana unaweza ukaona njia unayopita ni sawa lakini mwisho wake ni uharibifu mkubwa. Katika hili,mtu yeyote akiishi kufuata mwili kwa kile akionacho,atapotea tu. Biblia inazidi kutuambia kwamba “amebarikiwa mtu yule asiyekwenda kwenye njia ya wakosaji ” ( Zab.1:1). Hii ina maana kwamba, ikiwa utafanikiwa kuwakimbia watendao maovu kwa namna yoyote ile,kwa mfano kuwakimbia watu wenye mizaha,makundi ya watu wasengenyaji n.k,basi u heri wewe,yaani umebarikiwa.
Lakini ebu jiulize katika hili kwamba ni mara ngapi umekuwa ukishiriki vikao vya watu waovu? Ni mara ngapi unashiriki kupiga gumzo na waovu? Ujue jambo moja ya kwamba ikiwa kama utakuwa pamoja na watu wa namna hii mara kwa mara,basi ni lazima utashuka kiwango chako cha kiroho,na utamchukiza Bwana. Ninajifunza kitu ninapoyatafakari maisha ya Daudi mtu aliyeupendeza moyo wa Mungu. Lakini mtu huyo huyo,kuna kipindi alijisahau na kujikuta akiiacha njia ya Bwana kwa maana alilala na mke wa jemedari wake kisha akamuua huyo jemedari. Biblia inasema Daudi alitubu,kisha baada ya toba Daudi alitamani kutoka na kuwafundisha wakosaji waliokuwa wakitembea kwenye njia za mauti. ( Zab.51:13).
Daudi alitamani wakosaji wasije kuanguka zaidi kama alivyoanguka. Huu ndio moyo unaopaswa kuumbika ndani yako;kwamba unapowaangalia wakosaji utamani uwafundishe njia ya haki,ili waiche njia zao mbaya! Lakini,jihoji kwamba ndivyo ufanyavyo? Au ndivyo tunavyofanya leo? Kwa maana leo kile kinachofanyika ni kwamba kila mmoja ni mbinafsi hivyo tumejikuta wengi tunaomba Mungu atusamehe sisi tu na tukimaliza hatuna haja ya kuwaendea wakosaji ili na wao wasamehewe pia.
  • Njia ya haki ni ipi hiyo?
Neno “haki” kibiblia ni kuwa na uhusiano mwema na Mungu. Biblia inatusaidia kutupa maana ya “njia ya haki ” kwa kumweleza Yesu kuwa “Yeye mwenyewe ni njia” ( Yoh.14:6). Hii ikiwa na maana kwamba Yesu haoneshi njia,bali Yesu mwenyewe ndiye njia. Maana kuna utofauti ya mtu kuonesha njia na mtu binafsi kuwa njia.
Ikiwa Yesu mwenyewe ndiye njia hii ina maana mtu anayetaka kuja kwa Baba ni lazima tembee kwenye njia ambaye ndiye Yesu. Hivyo njia ya haki, ni utaratibu uliowekwa sahihi wa kutembea na Mungu. Ikiwa mtu mmoja akiita neno moja hili “wokovu” atakuwa hajakosea.Mungu ameweka utaratibu sahihi wa maisha kwa msaada wa Roho mtakatifu.
Kumbuka hili,mtu yeyote akiwa mbali na uso wa Mungu basi yupo mbali na njia ya haki. Na kwa sababu hiyo mtu huyo yupo huru mbali na haki. ( Warumi 6:20-21). Hii ina maana kwamba mtu ambaye yupo mbali na njia ya haki u mtumwa wa dhamb,na akiwa mtumwa wa dhambi basi ni sawa na kusema yupo na uhuru wa kutenda dhambi. Mfano; hujawahi kumwona mtu ambaye anaweza kujinyima kitu fulani ili makusudi atende dhambi? Au mtu ambaye yupo radhi apoteze gharama fulani kwa ajili ya kuipata dhambi fulani?? Ndio wapo,sasa watu wa namna hii ni watumwa wa dhambi nao wana uhuru mbali na haki.Ikiwa kama unahitaji kumwishia Kristo,huna budi kutembea kwenye njia ya haki kwa kuokoka kwanza kama sehemu muhimu sana.
Ifike wakati ujikague njia zako,upoje kwenye njia zako? Je upo kwenye njia ya Bwana? Je mfumo wa maisha yako unayoishi unampendeza Mungu? Vipi kama akija leo Kristo,utakwenda mbinguni au motoni,? Ukijihoji vizuri utagundua kwamba kuna mahali unahitaji kutengeneza na Mungu tena mapema kwa sababu usipofanya hivyo,lipo anguko mbele ya njia yako. Maneno haya ni muhimu kuyafanyia kazi.


July 31, 2019

IJUE BIBLIA | KUADABISHWA NA MUNGU

IJUE BIBLIA | KNOW THE BIBLE



KUADABISHWA NA MUNGU


Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi.
“kuadabishwa” ni aina ya nidhamu inayotolewa hasa na mzazi kwa mtoto wake. Kitendo hiki cha kumnyoosha mtoto aliyekosa ili aweze kumwelekea vyema babaye,au afuate utaratibu stahiki kwa upendo,huitwa “kuadabishwa “,hata hivyo; Biblia inalitumia neno hili kuonesha ya kwamba Mungu naye hutuadabisha kama njia ya kuturejeza kwenye mstari sahihi. Wakati mwingine biblia hutumia neno “marudia” kuwakilisha namna ya kuadabishwa.
Ukweli ni kwamba,yeyote unayempenda ni lazima utamrudi / yaani umfundishe nidhamu kwa bakola ya kumnyoosha kwa upendo kabisa . Na ikiwa kama hutoi nidhamu kwa mtu ambaye umpendaye,basi  haumpendi,kwa maana usipomfundisha nidhamu basi ujue atakuharibikia mkononi mwako huku ukimwona. Hata Mungu anatupenda sana,kiasi kwamba kwa pendo lake hataki tupotee au kuharibika kwa sababu hiyo inamlazimu atuchape kwa bakola za kibinadamu.
“ Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi,Naye humpiga kila mwana amkubaliye.Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye?“ Waebrania 12:6-7
Hakuna mwana asiyeadabiswa na babaye. Ebu fikiria kipindi cha utoto,ambapo baba yako alikuwa akikuchapa ili uende shule,na unapokosea kosea darasani baba alikuwa hakuachi bali anakuchapa na kukufuatilia sana huko shuleni wakati mwingine hutembea na bakola kucheki kama kweli umekwenda tuisheni au la,akigundua umetega hukwenda,basi hapo atakuchapa bakola mtindo mmoja. Lakini bakola hizo anazokuchapa atahakikisha hakupigi usoni,wala hakupigi ngumi ya uso,isipokuwa bakola za makalio. Kwa sababu anakupenda.
Lakini tazama sasa umekuwa mtu mzima na kwa bakola za mzee zimekufanya leo unaitwa msomi,zimekupeleka mahali fulani. Sasa katika mazingira kama hayo,fikiria kama mzee angekuchekea chekea pale ulipokataa masomo! Je leo hii ungelikuwa wapi? Ungeliitwa msomi? Lah hasha,ulihitaji bakola za baba yako zikufikishe hapo ulipo.
Ikiwa ndivyo,Mungu je? Maana Yeye hutupenda zaidi ya baba wa damu,hivyo ni lazima aturudi zaidi ili tufike kwenye eneo fulani zuri. Na ukumbuke kama Mungu anakuleta kwenye mstari sahihi lazima atakuchapa tu ila ni kwa fimbo ya kibinadamu kabisa, kwa mfano; unaweza ukajikuta unaumwa kama sehemu ya bakola ya Mungu ya kukurejeza ili ukae vizuri,ili usimtukane Mungu tena kwa maneno au matendo yako. Au unaweza unajikuta mambo yamefunga kila kona kama sehemu ya bakola ya Mungu ili urejee. N.K
Hata hivyo,tambua kwamba ; Kuadabishwa sio kuadhibiwa kwa maana neno “adhabu” lipo tofauti na neno “nidhamu “,kwa maana kupata adhabu huleta maumivu,mateso na kusababisha kulipa kisasi,isipokuwa kupata nidhamu kuna lengo la kumfundisha mkosaji kwa upendo,kwa lengo zuri kabisa tena pasipo kusababisha madhara. Mfano; mtoto anapokukosa na ukaamua kumsema au ukamchapa kwenye makalio kwa fimbo laini kwa lengo la kumfanya ashike adabu,huitwa unamfundisha nidhamu / unamwadabisha.
Lakini pale anapodiliki kumpiga mtoto hata kumuumiza,iwe kwa ngumi au makofi au kifaa chochote hata kusababisha uchungu na hasira ndani ya mtoto,hapo una mwadhibu/ hiyo huitwa “adhabu “. ( ebu fikiria unampiga mtoto kwa kuni au mwiko,au unamrushia jembe,huku ni kuleta madhara na ndio huitwa adhabu). Biblia haisemi kuwaadhibu watoto pale wanapokosea bali kuwapa nidhamu.
“Usimnyime mtoto wako mapigo;Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.” Mithali 23:13
Nasi tunapokuwa mbele za Bwana,tunastahili kuadabishwa ikiwa kama tunamkosea Yeye mwenye huruma. Wakati mwingine tunafikiria ni shetani,lakini si wakati wote;kwa maana njia zetu pia zinamhuzunisha Mungu, naye hutupatia nidhamu stahiki. Ebu chukulia mfano wa mtu ambaye anaijua kweli lakini hupenda kufanya dhambi tena anafanya hali akijua ni dhambi na kisha hufurahia dhambi, mtu huyu hawezi kuachwa vivi hivi,ni lazima apigwe kama nidhamu,ili asiizoee dhambi.
Kuna kipindi Bwana alisema na mfalme Daudi kwa habari ya uzao wake hasa Suleimani. Maana Daudi alitaka kumjengea nyumba Mungu, sasa Bwana akasema naye kwa kinywa cha Nabii Nathani. Akamwambia wazi wazi kwamba yeye Daudi hatajenga hekalu isipokuwa mwanae Suleimani ndiye atakayejenga,lakini akitenda uovu,atachapwa kama mkosaji;
“ Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu; akitenda maovu nitamwadhibu kwa fimbo ya binadamu na kwa mapigo ya wanadamu;” 2 Samweli 7:14
Bwana anapokuchapa haina maana hakupendi,bali ina maana anakupenda ndio maana unapewa bakola zako. Bakola hazifuti wala kuondoa pendo lake kwake,anakupenda tu,ingawa wewe hujali.
Kitu gani cha kufanya usipewe nidhamu (usiadabishwe)
  • Kujitahidi kutii.
Hakuna njia nyingine ya kukwepa kurudiwa isipokuwa ni katika kutii sauti yake na maelekezo yake yote. Na Mungu amewaweka wachungaji kusimama badala yake,wachungaji wasiposikilizwa maana yake sauti ya Mungu haikusikilizwa. Sasa ili usikie vyema utahitaji bakola zake kama sehemu ya mtoto mbele zake. Hivyo kabla ya kumkemea shetani,ni vyema ukatafakari njia zako maana wakati mwingine ni bakola tu zinakufanya hivyo na wala sio shetani. Ndio maana kabla ya kuanza maombi ya kubomoa na kuvunja kazi za ibilisi,anza na toba mbele za Bwana. Wengi leo wamechapwa kwa fimbo na Mungu na bahati mbaya wakidhani aliyewachapa ni shetani!
Lakini ukitafakari maisha yao kwa kina utagundua katika hayo yote kuna mkono wa Mungu pia kama sehemu ya kuwanyoosha ili warudi kwa Bwana kwa kuwa wamekuwa ni watu wa makosa ya mara kwa mara tena kwa makusudi kabisa. Tafakari sasa kwenye maisha yako,kisha ingia kwenye toba.