IJUE BIBLIA | LISTENING GOD'S VOICE THROUGH GOSPEL SONGS


Breaking News

Tuesday 24 May 2016

MAFANIKIO YA NDOA HAYATEGEMEI UPENDO TU:



MAFANIKIO YA NDOA HAYATEGEMEI UPENDO ZAIDI


Ndoa haifanikiwi kwa sababu ya UPENDO,

Hapo zamani kipindi wanawake walipokuwa hawaruhusiwi kufanya kazi wanazofanya wanaume,wanawake ilikuwa hata apigwe vipi anyanyaswe vipi hawezi kuondoka kwa mwanaume sio kwa sababu hataki au hawezi kuondoka ili ilikuwa kwa sababu za kiuchumi ni bora kuwa kwa mumewe kuliko kurudi kwao, na wanaume pia ilikuwa hawataki kukuza watoto na kazi za nyumbani. Mwanamke alimtegemea mwanaume na mwanaume alimtegemea mwanamke kila mmoja kwa faida yake.

Ila sasa mambo yamebadirika wanawake wana kazi na wanaume kazi ikifika jioni wote wamechoka, mwanamke hata akiondoka haoni kupungukiwa chochote ..bahati mbaya zaidi unamkuta ana nyumba yake ana gari lake ...ana maisha yake mazuri kuliko ya mwanaume.
“SIO UPENDO UNAO CHOCHEA KUWEPO MAHUSIANO YENYE MAFANIKIO”

Soma Biblia yako kwenye kitabu cha Mathayo 19: 3-6

Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu? Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke, akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja? Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.
TALAKA:

Hebu tukumbe kidogo miaka kama 40 kabla ya Yesu kuwepo alikuwepo nabii waliye muita Malaki,kipindi cha Malaki suala la TALAKA lilikuwa kubwa sana na lakutisha kwa sababu ya kitu kidogo tu mwanamke alikuwa anaachwa kwa TALAKA..mfano chafya kipindi cha kula,marafiki wa mwanamme wakija mwanamke akakaa muda mrefu sehemu walipo...talaka..n.k

Soma Malaki 2:13-
Tena mnatenda haya nayo; mnaifunikiza madhabahu ya Bwana kwa machozi, kwa kulia na kwa kuugua, hata asiiangalie tena hiyo dhabihu, wala kuitakabali mikononi mwenu na kuiridhia.
Hapa ukiangalia utgundua watu wengi ambao ndoa zao zimeharibika huwa wanakimbilia kanisani kuomba Mchungaji aombe ili NDOA ikae sawa..

Ukiangalia vizuri Mungu anacho zungumzia hapa utao “....mnaifunikiza madhabahu ya Bwana kwa machozi kwa kulia na kwa kuugua hata asiiangalie tena hiyo dhabihu ….

Ni kweli ni mtoaji mzuri wa sadaka kanisani hongera Mchungaji wako kakufundisha vyema na ukaelewa na ukatenda ni jambo zuri,ila swali wewe na mkeo mnaelewana,mnapatana,mnasemeshana?
Lakini ninyi mwasema, Ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu Bwana amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako, uliyemtenda mambo ya hiana, angawa yeye ni mwenzako, na mke wa agano lako.

Hivi unajua siku ulipokuwa unaoa huyo mkeo shahidi wa kwanza kufika kwenye harusi yako alikuwa ni Mungu wala haitaji mwaliko wako kwa kuwa wewe ni mwanae hakuna mtoto atumaye kadi ya mwaliko kwa baba yake kumualika harusini “...Ni kwa sababu Bwana amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako…” ukaapa nitakuwa naye kwenye shida na raha..alikuwa Mungu yupo anakusikiliza,Hivyo unapo oa/kuolewa maombi yako yanakuwa yanategemea kiapo chako kwanini rudi kasome Mathayo na Mwanzo vizuri “Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja

Kumbuka pindi unapoamua kuoa unaoa mtu wa kuzuia maombi yako usipokuwa makini utalia kila siku na kuomba bila majibu.
Mke ni mke wa Agano,hebu angalia kidogo Agano ni sawa na mkataba, unapo saini mkataba wowote huwa hauna hisia mkataba,ukisaini umesaini..
  
 Unaposaini mkataba wa ndoa hisia zako,mitazamo yako, yote inabadiliki inakuwa sio wewe tena bali ninyi..maana sio mmoja mmoja tena bali wa mmoja tu. 
 ....Naomba tukutane kesho kwa ajili ya muendelezo wa somo hili ni somo lefu sana ila naomba Mungu anisaidie nizidi kulifupisha kwa ajili ya kukusaidia kuelewa...
                                          Mungu Akubariki

No comments: