Mwanzo 1:26
“Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu ,kwa sura yetu wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya juu ya nchi.”
“Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu ,kwa sura yetu wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya juu ya nchi.”
1.Sura ya MUNGU..?
Sura ni nini?
Huwakilisha matendo yote yafanywayo na mwanadamu ndani ya mwili..akili.ufahamu,hekima,utashi,kuwaza,mtazamo n.k
2.Mfano wa MUNGU..?
mfano ni nini?
kwa kiingereza copy..kumbuka copy inafanana na original ila sio original,hivyo mwanadamu ana fanana na Mungu ila sio muungu..Muonekano,Mwenendo,Umbo..taswira.. kutembea, kuongea, mambo yote yamhusuyo mwanadamu yafanyikayo nje ya mwili
Wewe ni nani ambaye mbu uliyepewa kumtawala anakutawala mwili na akili zako kiasi cha kukata tamaa ya kuishi kabisa kwa sababu ya mbu...amka hapo wewe uliyeumbwa na Mungu uliye nafsi
SIFA ZA NAFSI
Fahamu hili hakuna mwili wenye jina, nafsi iliyopo ndani yako ndiyo yenye jina hilo uitwalo,mwili kazi yake ni kama bodi la gari lifanyalo kazi ya kupendezesha gari na kufunika engine ya gari na vifaa vingine vilivyo ndani ya gari bodi halifanyi gari itembee au isimame wala bodi likigongwa hausikii likilia kulalamika maumivu ila wewe uliyendani ya bodi la gari.
hivyo wewe ni nafsi na mwili ni bodi...mwili hausikii maumivu nafsi ndo inasikia maumivu..maumivu hayo huyapokea kutoka kwa mwili kupitia macho,masikio,ngozi,pua na ulimi..ulisha wahi kujiuliza ni kwanini wakati mwingine hata ukijikwaa husikii maumivu mpaka macho yaone damu ikitoka? Au ulishawahi kuona maiti ikilalamika baridi mwochwali au kuchomwa moto au ulishaona ikisikia maumivu popote iguswapo na kitu chenye ncha kali? sababu ni maiti haina nafsi ni gari chakavu lisilo na engini wala vitu vya ndani halifanyi kazi......
Nini nataka kusema nafsi yako ikikataa ugonjwa ulio nao kwa kuwa nafsi haiumwi wala haifi bali mwili ndo wenye kuumwa na kufa na mwili wako hauna nguvu ya kutawala nafsi usipoupa nafasi....wengi wenu mnaumwa kwa sababu miili inaendesha ingine kituambacho hakitakiwi kwa kuwa hakuna kiwanda kinachotengeneza gari liendeshwe na bodi...
Badili mtazamo wako leo usimame hapo ulipo huna haja ya kuchosha watumishi wa Mungu kwa magojwa ambayo tiba yake ni kuamini kuwa nafsi yako haiumwi na mwili hauna nguvu juu ya nafsi yako ukiamini amuka hapo ulipolala na uende kanisani ukamshukur Mungu kwa kuwa umzima wewe...
Sema Amen!!!!!
No comments:
Post a Comment