IJUE BIBLIA | KNOW THE BIBLE
TUMAINI KATIKA MUNGU
Warumi 15:13 Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
13 Mungu wa tumaini awajaze ninyi furaha na amani katika kumwamini, ili kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, mpate kuwa na tumaini tele.
Mungu pekee ndie aliyeziumba roho zote kama tunavyosoma katika maandiko ya kale, hivyo yeye anajua sababu ya kila mmoja kuwepo hapa duniani na kuwepo mahala alipo yeye pekee ndie awezae kuwapa wanadamu tumaini la kwali kwakua tunajua hajawahi kusema uongo na ni mwaminifu anatenda.
Mungu huyu amefanyika katika Roho na amekuwa mmoja na mwnadamu kwa kuifanya roho ya mwanadamu kufanana na yake. Hivyo Roho wa Mungu ambae ndie Mtakatifu anaendelea kuhusika na maisha yako katika kila unalopitia.
Nakutakia Tafakari njema na karibu kushirikiana nami katika kujifunza.
Kila siku upate tafakali ya Neno la Kristo.
Mungu wa Mbinguni, mwenye nguvu na akutoe mahali hapo ulipokwama mpendwa, tazama Yeye, tazama amani ya Kristo na ijae ndani yako, huzuni isiwepo ndani yako tena,
Tunakushukuru Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu kwa kuwa amani yenu i ndani yetu sasa na hata milel.
wote tuseme Amen.
No comments:
Post a Comment